Saturday 8 October 2016

Jela kwa kukutwa na hatia ya kumlazimisha mwanaume mwenzie amnyonye sehemu za siri

Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemhukumu kifungo cha maisha jela, Erick Kasila (39) baada ya kupatikana na hatia katika mashtaka matatulikiwamo la kumlawiti mwanamume kwa madai kuwa alimfumania gesti na akiwa na mke wake.

Kasila anadaiwa kumlawiti Idd Kambi katika nyumba ya kulala Wageni ya Maembe, Yombo Kiwalani, Wilaya ya Ilala na kumpiga picha za utupu na kutisha kunitumia katika mitandao ya kijamiina kumnyang’anya nguo alizovaa, fedha, laptop na viatu.

Mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo, Juma Richard (31) alihukumiwa kifungo cha miaka 14 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlazimisha mlalamikaji kumnyonya uume wake na kumtaka kusaini karatasi ya ahadi ya Sh1 milioni ili asisambaze picha walizompiga wakati wakimlawiti,ambazo hata hivyo, walizisambaza katika mitandao ya kijamii.

Akisoma hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Said Mkasiwa alisema ameridhishwa na ushahidi wa mashahidi watano dhidi ya washtakiwa na vielelezovya picha zinazoonyesha mlalamikaji alikuwa analawitiwa,nyingine zikionyesha mshtakiwa akimlazimisha mlalamikaji amnyonye sehemu zake za siri.

Akipitia baadhi ya ushahidi uliotolewa mahakamani hapo, Hakimu Mkasiwa alisema kulawitiwa kwa mwanamume huyo ni baada ya kukutwa na Sanifa Bakari ambaye ni mke waKasila.

Kabla ya hukumu hiyo, upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Silvia Mitanto uliiomba Mahakama kutoa adhabu kali dhidi ya washtakiwa hao kwa kitendo walichokifanya ambacho kimemuathiri mlalamikaji kisaikolojia.Washtakiwa walipopewa nafasi ya kujitetea kwa nini wasipewe adhabu kali, walishindwa na badala yake waliomba nakala yahukumu.

Mwananchi

Wednesday 17 August 2016

Ndoa ya Masanja yaingia doa, asakwa na polisi akituhumiwa kumiliki sare za polisi

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linamsaka Emmanuel Mgaya maarufu kama, Masanja Mkandamizaji ambaye ni msanii wa vichekesho wa kundi la Orijino Komedi kwa tuhuma za kumiliki sare za jeshi hilo jambo ambalo ni kinyume na sheria, anaandika Pendo Omary.

Wakati Masanja akisakwa, tayari wasanii wenzake akiwemo, Lucas Lazaro (Joti), Serious David na Alex John wanashikiliwa na jeshi hilo kwa mahojiano baada ya kuonekana katika mkanda wa video wakiwa wamevaa sare zinazodhaniwa kuwa ni za jeshi hilo.

Hezron Gyimbi Naibu Kamishina wa Polisi na Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, amewambia wanahabari kuwa, wasanii hao walikamatwa Jana (juzi) saa 10 jioni.

“Walikamatwa kwa kosa la kuvaa sare zinazodhaniwa kuwa ni za Polisi ambazo ni kofia, suruali, shati, mkanda, filimbi na beji yenye cheo cha Polisi.

“Lengo letu ni kutaka kujua, walizipata wapi sare hizo na kuangalia uhalali wa kuwa nazo pamoja na kuchunguza kama hawana vifaa vingine vya Polisi tofauti na hivi walivyokamatwa navyo,” amesema Gyimbi huku akiongeza kuwa;

“Dhamana ya watuhumiwa hao ipo wazi iwapo watatimiza masharti huku upelelezi ukiendelea na watakapohitajika kwa ajili ya hatua nyingine wataitwa,”.

Wasanii hao walionekana katika video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii mwishoni mwa wiki iliyopita, wakiwa wamevalia sare zinazodhaniwa kuwa, ni za Jeshi la Polisi katika harusi ya Masanja.

Jambo lililoibua mijadala kuhusu uhalali wa sare hizo kutumiwa kiholela.

Mwanahalisi

Nafasi ya kazi Medical Officer

NAFASI YA KAZI MEDICAL OFFICER STAMIGOLD COMPANY LIMITED

Is a subsidiary Company of the state mining cooperation STAMICO operating the gold mine.  The mine is located in the Biharamulo forest reserve, south west of Mwanza  in Kagera Region.  In order to run the mine effectively and efficiently the company invites applications from qualified candidates to fill the existing vacancy detailed below

Work station                                       Biharamulo Mine site

Work Roster                                        6/342 days on 21 days of

Contact Duration                              not exceeding 2 years subjected to renewal

THE ROLE MODEL:

-          Medical Officer will be reporting to the clinic Supervisor ensuring the clinic delivers a high standard  of patient care provided by the nursing , also will ensure good working knowledge and utilization of clinic

DUTIES AND RESPONSIBILITIES:

-          Providing health care on daily basis including normal an on call consultation, providing medical advice to employee, infectious diseases, diseases out break vaccination and travel advice,

-          Participating the physical medical evacuation process by road or air as circumstance require,

-          Implement all occupational health program, employee, assistance, programs, Malaria  control program, health promoting  program and HIV/AIDS control,    

-          Involved in planning and implementation of health promotion activities, delivery of awareness session/ training to employee,

-          Decisiveness, resilience and resourcefulness with high degree of confidentiality,

-          Strong and proven management ability with leadership qualities are essential,

-          High level of interpersonal skills team player, flexible, attentive, to eletalis result oriented.  

 

QUALIFICATIONS:

-          A holder of doctor of Medicine degree from any recognized University,

-          Maintaining clinical registration to practice in Tanzania,

-          A minimum of 3 years of working experience in medical practice  post internship,

-          Experience in mining industry is an added advantage,

     MODE OF APPLICATION

   Interested applicants meeting the above job requirements should send their applications with their curriculum vitae either photocopies of birth certificate or vote certificate id or travel passport, copies of academic qualifications and provides names of 3 referees with their contacts, postal address e- mail and telephone number

APPLICATIONS should be addressed to the under mentioned not later than 28 August 2016

Hr.biharamuro@stamigold.co.tz

Or

GENERAL MANAGER,

P.O. BOX 78508,

DAR ES SALAAM

Nafasi ya kazi, Chief Surveyor, mwisho wa kutuma maombi Agosti 29, 2016

NAFASI YA KAZI CHIEF SURVEYOR TANZANITE ONE MINING

Tanzanite one mining is looking for Chief Surveyor and we would like to invite applicants who can fulfill the following job requirement

Job location                Mererani   Manyara

The role will involve managing and performing a range of surveying duties both and underground which is physically demanding environment.  The role will suit anyone with dynamic and enthusiastic attitude who wants to utilize their skills as surveyor to ensure success of the company.  It will be important that the candidate can work as an effective member of multicultural team.  Experienced candidates only need to apply

DUTIES AND RESPONSIBILITY

-          The surveyor is responsible in planning day to day survey activities of the mine including underground and surface

-          Preparation of monthly and mid-month survey measuring and compilation of results

-          Updating of date on Micro mine and plotting of data on micro mine

-          Ensuring grade and directions is adhere to by the miners

-          Training of surveying staff in calculations equipment usage. etc

  QUALIFICATIONS AND SKILLS REQUIRED

-          Degree in surveying from a recognize university

-          Fluency in English and Swahili

-          Ability to use a variety of surveying equipment particular a total station

-          Previous mining experience essential not less than 5 years

-          Previous working knowledge of mining software  such as micro mine(proffered) or surpac/ data essential

-          Excellent computer skills particularly in ms Office essential

-          A good  degree of finites is required due to the physical nature of the work

   Candidates interested in applying should send a covering letter and their CV to hr@tanzaniteone.com

Application will not be accepted after the 29th August 2016

Source Mwananchi 17 August 2016

Tuesday 2 August 2016

Hofu yatanda baada ya fisi kumng'ata mtoto makalio

Wakazi wa kitongoji cha Minjaleni kata ya Mpapura mkoani Mtwara wameiomba Serikali kumthibiti fisi anayezunguka kwenye kata hiyo, baada ya kumjeruhi vibaya kwa kumg’ata kwenye makalio, mtoto wa miaka 8 Astara Hamis mwanafunzi wa darasa la 1, na pia kuua mbuzi 20 katika kipindi kisichozidi miezi 2.

Mwenyekiti wa kitongoji hicho Issa Mshamu amesema kufuatia kutokea ghafla kwa fisi huyo anayezunguka nakujeruhi, wananchi wamekuwa na hofukubwa na kushindwa kufanya shughuliza maendeleo ikiwemo kwenda kuvuna mtama mashambani, ikizingatiwa huu ni wakati wake wa uvunaji wa zao hilo.

Kwa upande wake, mama mzazi wa mtoto Astara Hamisi Bibi Fatuma Mataka amesema mwanae alishambuliwa na fisi majira ya saa 12.30 jioni alipokwenda na watoto wenzake mto  mambi kuoga, lakini aliokolewa na wananchi wakati fisi huyo akimburuzia mtoto huyo porini.

Alipoulizwa juu ya hali hiyo, diwani wakata ya Mpapura Maupa Bakari amekiri kuwepo kwa tishio kubwa la fisi kwenye kata hiyo na kumjeruhi vibaya na fisi kwa mtoto Astara, na hivyo amesema,mbali na tukio hilo kufikishwa kwa viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Mtwara, mipango anaifanya yeye kama diwani ya kumtega fisi huyo kwa nyavu.

Itvhabari