Wednesday, 1 June 2016

Ulevi huu ni noma, fuatilia kilichomkuta huyu baada ya kulewa

Furaha ya pombe iligeuka majonzi baada ya Joseph Simon (39), kuuawa kwa kuchomwa kisu na mnywaji mwenzake.

Simon ambaye ni mkazi na mkulima wa Kijiji cha Mkiwa wilayani Ikungi, Mkoa wa Singida, alikumbwa na mkasa huo alipokuwa kilabuni wakinywa pombe na mtu huyo (jina linahifadhiwa).

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka alisema mauaji hayo yalitokea Mei 28, saa 1.30 jioni katika kijiji hicho.

Sadoyeka alisema siku ya tukio, Joseph alikwenda nyumbani kwa mtu huyo kwa ajili ya kunywa pombe ya kienyeji aina ya mtukuru na ndipo alipokumbwa na mkasa huo.

“Wakazi hawa wawili wa Kijiji cha Mkiwa ambao walikuwa hawana uhusiano wowote, baada ya kulewa pombe walianza ugomvi ambao sababu yake haijafahamika. Ugomvi huo ulisababisha (mtu huyo) aingine ndani na kutoka na kitu chenye ncha kalina kumchoma mdomoni Joseph na kufa papo hapo, ” alisema Kamanda Sedoyeka.

Alisema wanamshikilia mtu huyo kwa tuhuma za mauaji na watamfikisha mahakamani kujibu mashtaka.

Mwananchi