Kumbe ni muhimu sana kwa wanawake kutembea na japo upande mmoja wa khanga kwa ajili ya kujistili pindi wanapopata tatizo kama hili.
Dada mmoja ambaye jina lake alikuweza kupatikana, maeneo ya mwananyala "A" amejikuta akikumbwa na aibu baada ya kugundua zipu ya gauni lake imeachia na kukosa cha kujistili hadi msamalia mwema alipotokea na kumstili na upande wa khanga.
Aligundua hilo baada ya kuambiwa na mpita njia kwamba zipu yake imeachia na kuanza kujiskia vibaya na kushikwa na wasiwasi hadi pale aliposaidiwa upande wa khanga na msamalia mwema.