Dunia haiishi vituko. Mfanyabiashara maarufu wa nyumba za kulala wageni mjini hapa, Charles Soka ambaye ni shabiki wa Timu ya Simba amefanya sherehe ya kuwapongeza wanachama na mashabiki wa timu ya Yanga mkoani hapa kwa kufanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom.
Akizungumza katika sherehe hizo jana , soka ambaye ni mkurugenzi wa Nakite Lodge, amesema ingawa yeye ni mshabiki mkubwa wa timu ya Simba, lakini ameguswa kuwafanyia sherehe mashabiki wa Yanga kutokana na mafanikio makubwa waliyopata mwaka huu.
Soka amesema pamoja na timu hiyo kuchukua ubingwa wa ligi kuu,pia imefanikiwa kutwaa ubingwa wa chama cha soka nchini (FA) pamoja na kuingia katika hatua ya makundi ya mashindano ya shirikisho barani Afrika.
''Mimi binafsi naamini mpira ni furaha, ingawa ni mpenzi mkubwawa Simba, nimeona vyema kuwapongeza watani zetu Yanga kwa mafanikio waliyopata msimu huu, naamini msimu ujao itakuwa zamu yao kutupongeza,” amesemahuku akicheka.