Wednesday, 1 June 2016

Tiffah mtoto wa Diamond Plutinumz akimbiza BET

Kituo cha runinga cha BET Afrika kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii huwa kinakuwa na programu ya kuposti picha za watoto wa wasanii maarufu Afrika.

Programu hiyo ambayo imepewa jina la Our CuteDay snap wiki hii imemwangukia mtoto wa Diamond Platinumz Tiffah ambapo kituo hicho kimeposti picha ya Tiffah katika mitandao yake ya kijamii kama CuteDay snap ya wiki hii.

Posti hiyo ilisomeka hivi

"Our #CuteDay snap is baby Princess Tiffah, @diamondplatnumz’s bundle of cuteness. RT to share the cuteness,” wameandika BET kwenye picha ya mtoto huyo iliyowekwa Instagram na Twitter.

Umaarufu wa Diamond Plutinumz sasa unaamia kwa mtoto wake wa pekee ambaye nae anaonekana kufuafa nyota ya umaarufu aliyonayo baba yake.