Wednesday, 19 November 2014

Young Killer: Sipo chini ya mtu wala studio tena, najisimamia mwenyewe

Rapper Young Killer Msodoki amesema kwa sasa yeye ni msanii anayejisimamia mwenyewe na wala hayupo chini ya mtu wala studio.

Young Killer ameiambia Bongo5 kuwa mkataba wake na Mona G walishauvunja kutokana na sababu ambazo hakupenda kuziweka wazi.

“Mpaka sasa hivi sipo kwa Mona na mkataba naweza kusema umeisha. Sasa hivi nafanya kazi mimi kama mimi najisimamia mwenyewe na kazi zangu na zinaenda kama kawaida na hakuna utofauti wowote kati ya mwanzo na sasa hivi.

“Maisha ni yale yale na mambo yangu ni yale yale, mkataba wangu tuliusitisha tu, kwahiyo kila mtu anafanya kazi kimpango wake. Mkataba wetu tuliusitisha tangu mwezi wa saba lakini ulikuwa katika utofauti na mwanzo, sasa hivi kama nina kazi kwa Mona ninafanya kwa kulipia,” alisema Msodoki.

Via Bongo5.com