Serikali wilayani Mpanda mkoani Katavi imeonya tabia ya baadhi ya wazazi ambao wanahonga baadhi ya walimu wa shule za msingi na sekondari ili wawafute watoto wao wa kike katika orodha ya wanafunzi kwa kisingizio kwamba wamekufa ili waweze kuwaoza.
Karipio hilo kwa walimu na wazazi, limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Paza Mwamlima juzi wakati akiwahutubia wananchi wilayani humo wakati wa maadhimisho ya Sherehe za kutimiza Miaka 20 ya Chama Kikuu cha Ushirika cha Wakulima wa Tumbaku cha Mkoa wa Katavi (LATCU), yaliyofanyika mjini humo.
Mwamlima alisema kuna tabia kwa baadhi ya wazazi na walezi, ambao wanadaiwa kushirikiana na walimu katika mchezo huo mchafu wa kukatisha masomo ya wanafunzi wa kike kwa kuwapa ‘hongo’, ikiwemo fedha na mifugo ili wafutwe katika orodha ya wanafunzi wa shule zao ili waweze kuozwa.
Via HabariLeo