Mada iliandikwa hivi
"Ni katika Morning Jam Leo Jumatano November 19...Licha ya serikali kutoa nafasi kwa wananchi kujiunga na mafunzo ya jeshi la kujenga taifa lakini changamoto kubwa ni ukosefu wa ajira kwa wahitimu wa mafunzo hayo Jambo linalohatarisha usalama wa nchi kutokana na baadhi ya askari waliopitia JKT kujiunga na makundi mbalimbali ya uhalifu Je nini kifanyike kudhibiti hali hii?"
Maoni ya wachangiaji
Neema Kimario
kutoka arusha unga ltd...habari zenu studio...yaan sijui kama kuna sekta ambayo haina lawama hapa nchin, utafrikiri hatuna serikali,kuhusu maada mezani mi naona serikali ifanye kila njia kuhakikisha ajira inapatikana kwa hawa wahitimu, tofauti na hivyo, tutajaza vibaka na majambazi nchin..asubui njema b na mihambo
Edited · Like · 48 · Reply · 55 minutes ago
2 replies
David Mnenegwa Juniour
tOKA WAZALENDO INC TEAM MBEZI LUIS DSM
Habari gani Ndani Ya Morning Jamz..?
Kwa kweli hili swala lipo tena ni hatari sana kwa taifa wamewapeleka Vijana Jeshini siku hizi Vijana Wanaweza kutumia Zana,Risasi za Moto na N.k
Halafu hawajawapa Ajila hao vijana Wamekuja huku Uraiani imekuwa hatari sana kwani wamekuwa Wajasili na Wakakamavu basi ndiyo hao hao wengi wao Wamekuwa Majambaz, Vibaka Na Polapola ni hatari sana Mitaani kwetu
Embu serikali iamue swala Moja kuwaita na kuwapa Ajila ili kuokoa Maisha yetu Wanyonge Au kusitisha kutoa Mafunzo Ya kijesh kwa Vijana ni hatari sana
Call me David Mnenegwa Master Stater frm wazalendo Inc team mbez bengaa
Edited · Like · 41 · Reply · 1 hour ago
Henry Joseph Mushi Kitunguu
Kutoka Watifu Classic Ngateu Arusha! Kwanza Niwajulie Hali Hapo Studio B Na Mihambo/
Ni Vyema Serikali Ikalichukulia Swala Hili Kwa Uzito Zaidi! Mana Kijana Anapomaliza Mafunzo Yake Anategemea Kupata Ajira! Na Endapo Atakosa Ajiraaa Ndipo Tunakujakuona Makundi Yenye Kuhatarisha Maisha Ya Watu Mana Ni Lazima Uhalifu Uongezeke. Kazinyema Kwenu
Edited · Like · 41 · Reply · 23 minutes ago
Hawa Wa Omary
1st lady wa Ngaramtoni ya Juu Arusha Serekali ijipange tena saana na kuhakikisha wanapomaliza mafunzo haraka wapatiwe ajira kwani bila kufanya hivyo wataendelea kujiunga na mskundi ya kigaidi ili wajipatie pesa.Asubuhi Njema
Like · 22 · Reply · 1 hour ago
Moussa Matua
Kikubwa ni serikar kubuni mbinu za kuwafanya hao wanajeshi kutumika... serikali iamini tu tuna janga la kiuchumi hivyo ni vyema pia jeshi kutumika ili kujikwamua kiuchumi wa wao na taifa kiujumla. Zipatikane sekta na fursa mbali mbali kwa mikakat yenye manufaa sio kuwaachia mtaani huku hawajawapa elimu ya kujiajir
Like · 1 · Reply · 1 hour ago
Via CapitalRadioTanzania facebook page