Tuesday, 15 April 2014

(Picha): Kampuni ya US Airways yatuma tweet yenye picha ya ngono.

Kampuni ya usafirishaji ya ndege ya Marekani ya US Airways imeomba msamaha kwa kutuma tweet yenye picha ya ngono kwenye ukurasa wao wa twitter wakati wakijaribu kumjibu mteja wao.

Kampuni ilisema kuwa, walikuwa wanajaribu kurekebisha makosa fulani ndipo wakajikuta wanaituma tweet hiyo kimakosa.

Tweet hiyo ilikuja kufutwa saa moja baadae baada ya kutumwa 'retweeted' karibia mara mia moja.Kampuni imesema kuwa inasikitishwa sana na tatizo hilo.

Picha hiyo ya uchi yenye picha ya mwanamke na kitoi cha ndege (kwenye picha) kwa mara ya kwanza ilitumwa na mteja wa kampuni hiyo kuwaelezea jinsi kampuni nyingine ilivyomkera na usafiri wao kwa kumchelewesha.

Kampuni ina wafuasi zaidi ya 420,000 na tangu tukio litokee hawajatuma tweet nyingine.