Tuesday, 15 April 2014

Mwanasiasa wa India asema mwanamke anayefanya mapenzi kabla ya kuolewa anyongwe.

Kiongozi mmoja wa chama cha siasa nchini India cha socialist party, Abu Azmi, ameishangaza dunia kwa kusema kuwa wanawake wote wanaofanya mapenzi kabla hawajaolewa wanatakiwa kunyongwa.

Alisema kuwa hata kama dada huyo atakuwa amebakwa wakati bado hajaolewa pia nae anastahili kutiwa kamba.

Mwanasiasa huyo alisema kwamba, kutokana na sheria za kiislamu zinavyosema anapaswa kuhukumiwa kifo iwe ameshiriki kwa kutaka mwenyewe ama la.

Abu Azmi aliyasema hayo kujibu maoni ya mkuu wa chama chake Mulayam Singh Yadav, aliyesema adhabu ya kifo kwa wabakaji ni kali mno kwa kuwa vijana hao wanakosea tu.