Tuesday, 11 March 2014

Wanaharakati waicharukia sheria ya kuzuia ushoga Uganda. Ebu fuatilia hapa upate kufahamu kinachoendelea huko Uganda.

Wanaharakati wa wapenzi wa jinsia moja, mawakili na wansiasa wamewasilisha kesi mahakamani nchini Uganda kupinga sheria
mpya dhidi ya mapenzi ya jinsia moja nchini humo.

Wanaharakati hao, wanasema kuwa sheria hiyo inakiuka katiba ya Uganda na kuendeleza ubaguzi na kukandamiza uhuru wa kujieleza.

Sheria hiyo ilitiwa saini na Rais Yoweri Museveni mwezi jana na imelaaniwa vikali na jamii ya
kimataifa.

Rais wa Marekani Barack Obama ameitaja sheria hiyo kama hatua ya ukandamizaji kwa waganda
na nchi kadhaa tayari zimetishia kuinyima Uganda msaada.

Mwandishi wa BBC mjini Kampala anasema kuwa itachukua miezi kadhaa kabla ya kusikilizwa.