Tuesday, 11 March 2014

Kwa nini umkemee mtoto kwa kutumia matusi!? Hii hapa AMSHA AMSHA na vitendo, ifuatilie hapa upate mengi zaidi.

Kwa nini unamkanya mwanao kwa kutumia matusi? Je, unategemea mtoto huyu atajifunza nini toka kwako kama si matusi? Uoni kama unamrithisha matusi?

Ni tabia iliyo sugu sana miongoni mwa wazazi kwa watoto wao bila kufahamu kuwa wanajenga tabia ya utumizi wa matusi kwa watoto wao.

Urithi huu anaoupata mtoto toka kwa mzazi na kukua nao unaifanya akili yake iwe imetawaliwa na matusi huku akiyafyatua na kuyanukisha mahali popote bila kujali amezungukwa na nani.

AMKA mzazi, acha kumkemea  mtoto kwa kutumia matusi.