Friday, 14 March 2014

Rais wa klabu bingwa Ulaya, Beyern Munich, atiwa hatiani kwa utapeli. Mfuate vitendo hapa upate kufahamu zaidi juu ya hili.

Mahakama nchini Ujerumani imemhukumu rais wa klabu bingwa Ulaya, Bayern Munich, Uli
Hoeness, kifungo cha miaka mitatu na miezi sita jela kwa kukwepa kulipa kodi.

Nyota huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 62 alikiri kuitapeli mamlaka ya kutoza ushuru ya
Ujerumani mamilioni ya Euro huku akiweka akiba ya fedha zake kisiri kwenye akaunti ya benki ya
Uswizi.

Licha ya wakili wake kuiomba mahakama kutomwadhibu Bw Hoeness kwa sababu ya
kujisalimisha kwake, mahakimu waliafikia kwamba Hoeness hakukiri kikamilifu.

Hapo awali Hoeness alishtakiwa kwa kukwepa kulipa ushuru wa euro milioni 3.5 (£2.9m;
$4.9m) lakini baadaye akakiri kuwa hajawahi kulipa milioni nyingine 15.

Hatimaye Alhamisi, korti ilibaini kuwa alikosa kulipa ushuru wa jumla ya euro milioni 27.2.

Hoeness amesema hatakata rufaa dhidi ya uamuzi huo. Hata hivyo Hoeness atabakia kuwa huru hadi
uamuzi wa mwisho kabisa utakapotolewa.