Hakimu anayesikiliza kesi ya Chris Brown dhidi ya kosa linalomkabili la kumpiga Rihanna inakumbukwa kuwa alimwamuru Chris kwenda Rehab kwa siku 90 kupata matibabu ya kupunguza tatizo la hasira alilonalo.
Lakini inaelezwa kuwa mapema jana ijumaa Chris alifukuzwa Rehab na kutupwa jela kwa kosa la kuvunja sheria za Rehab ambazo hazikuwekwa wazi.
Iliamuliwa kuwa endapo Chris ataondolewa Rehab, basi atatupwa jela moja kwa moja, vyanzo mbalimbali vililipoti.
Bado haijafahamika jambo gani alilolifanya Chris. Vyanzo vinasema kuwa kosa hilo alilofanya halihusishi madawa wala fujo.
Pia vyanzo vinasema, Chris alikamatwa akiwa na mahusiano mabaya na mmoja wa wanawake wanaofanya kazi Rehab jambo ambalo pia limeelezwa sio sababu iliyomfanya afukuzwe Rehab. Huyu jamaa amefanya nini? Endelea kuwa pamoja na vitendo ili upate jibu la swali hilo hapo baadae.