Tuesday, 18 March 2014

Polisi 4 watimuliwa kazi Dar, majina yao pia yapo hapa, mfuate vitendo hapa.

Jeshi la Polisi Jijini Dar es Salaam limewafukuza kazi askari polisi wanne kwa makosa ya kuhusika
katika uhalifu.

Askari hao ni Rajab Mkwenda mwenye namba E 6396 wa polisi makao makuu, Saimon F 9412 wa
kituo cha kati, Albas Poosa F 9414 wa bendi ya polisi Dar na Suleiman F 9512 wa Kigamboni.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,
Kamishna Suleimani Kova alisema askari hao wamekuwa wakihusika katika uhalifu ikiwa ni pamoja na tukio la majambazi 15 waliovamia
kampuni ya Kichina ya Hong Yang iliyopo Mbezi Beach A.

“Hatua iliyochukuliwa na polisi kuwafukuza kwa fedheha inawastahili kutokana na kulidhalilisha Jeshi la Polisi na wamefukuzwa kazi kuanzia
tarehe 17 Machi na hatutavumilia vitendo vya ukiukwaji wa maadili” alizema Kamishina Kova.

Alisema majambazi hao walipora vitu mbalimbali ikiwemo simu na fedha na kugundulika kuwa
baadhi ya majambazi hao ni askari polisi ambao nao walishiriki katika tukio hilo.

Kova aliongeza kuuwa, jalada la kesi hiyo pamoja na majalada mengne yatapelekwa kwa
Mwanasheria Mkuu wa Serikali kabla ya kuwafikisha mahakamani askari hao kwa makosa ya jinai.

Katika hatua nyingine, Kamishna Kova alisema wamefanikiwa kukamata tindikali lita 21 maeneo
ya Vingunguti Miembei wilayani Ilala katika chumba cha mkazi mmoja wa eneo hilo ambaye
hakuwapo chumbani wakati huo na upelelezi unaendelea ili kumtambua na kumkamata .

Kamishna Suleimani Kova