Friday, 14 March 2014

Mtoto aliyezaliwa na vichwa viwili, mwili mmoja, uti wa mgongo mara mbili. Ebu mfuate hapa vitendo ukaone na kupata taarifa juu ya mtoto huyo.

Mwanamke wa kihindi, Urmila Sharma (28) amejifungua watoto mapacha wenye vichwa viwili lakini mwili mmoja. Alijifungua juzi jumatanno.

Imeelezwa kuwa wakati wa ujauzito, Urmila hakuwa na uwezo wa kugharamia huduma ya uchunguzi (ultrasound) ili kujua anabeba watoto mapacha walio salama au la. "Mtoto huyo wa kike kwa sasa ni mwenye afya," Dr. Ashish Sehgal alisema. Aliongeza kuwa mtoto huyo ambaye ana vichwa viwili na mwili mmoja ni vigumu sana kumtenganisha kwa sasa hadi pale atakapotengamaa na kuangalia mgawanyiko wake viungo ukoje. Mtoto huyo alizaliwa na kilo 7 akiwa na vichwa viwili na uti wa mgongo uliogawanyika sehemu mbili (two spines).