Sunday, 16 March 2014

Majonzi ya Rooney haya hapa kufuatia kipigo toka kwa Liverpool. Fuatana na vitendo hapa upate kujua maneno yaliyomtoka Rooney.

Mshambulizi wa Manchester United Wayne Rooney amesema kuwa kipigo cha mabao 3-0
walichokipata kutoka kwa Liverpool ni kama janga kwake na hiki ndio kipindi kigumu kwake kuwahi kukishuhudia tangu kuanza kucheza soka ya kulipwa.

Steven Gerrard alifunga mabao mawili kutokana na mikwaju miwili ya penati na kukosa la tatu
kabla ya Luis Suarez kuongeza bao la tatu.

Rooney mzaliwa wa Liverpool mwenye umri wa miaka 28, amesema kuwa hiki ni kipindi kigumu sana kwake na wembe ambao hautoshi hata kumezwa.

"Hili ni jinamizi . Ni siku mbaya sana kwangu, sijawahi kuhisi vibaya kama hivi maishani mwangu
nikicheza mpira. Yaani hata vigumu kutafakari. Liverpool
ilicheza vizuri sana , lakini hii ni hali ngumu kwangu, '' alisema Rooney.

''Hakuna anayetaka kushindwa hapa hasa katika uwanja wa nyumbani, sio vizuri.'' Rooney alisema.

Rooney katika mechi hiyo, alipata nafasi moja tu ya kujaribu
kuingiza bao katika mechi hiyo ambayo Liverpool ilidhibiti tangu mwanzo ingawa hakufanikiwa.