Sunday, 2 February 2014

WAZAZI MBARONI KWA KUWANYIMA WATOTO WAO HAKI YA MSINGI.

Wazazi 18  wilayani Muleba mkoani Kagera, wanashikiliwa na polisi baada ya kukaidi agizo la mkuu wa wilaya la kuwatimizia watoto wao haki ya msingi ya kuwapeleka kujiunga na kidato cha kwanza.

Wazazi hao walikamatwa baada ya kubisha agizo la mkuu wa wilaya hiyo, Lembris Kipuyo la kuwapeleka watoto wao shuleni hata kama hawana ada na vifaa vingine.

Kipuyo alisema,msako wa kuwatia nguvuni wazazi wemgine ambao hawajawapeleka watoto wao shuleni hadi sasa bado unaendelea ndani ya kata zote wiayani humo.

Kipuyo aliongeza kwa kuwasisitiza wazazi na walezi ambao hawajawapeleka watoto wao shuleni kuwapeleka hata kama hawana ada na michango mingine ili waweze kutafutiwa namna ya kuwasaidia kupata mahitaji hayo huku wakiendelea na masomo.

Chanzo,nipashe.