Mbaya sana!!! Kundi la vijana wadogo wenye umri chini ya miaka kumi na nane (18) limekuwa tishio kwa wananchi wa maeneo ya Kiwalani Dar es salaam kutokana na kundi hilo kujihusisha na ukabaji,uporaji pamoja na kujeruhi pia.
Kundi hilo linalojulikana kama watoto wa mbwa mwitu limetengeneza hofu mingoni mwa wakazi wa maeneo ya Kiwalani pamoja na Yombo kwa kuhofia kuheruhiwa.
Kundi hilo linaloundwa na vijana walio chini ya umri limepelekea pia hofu kwa wamiliki wa maduka maeneo ya Kiwalani na Yombo kwa kufunga maduka yao tofauti na muda wa kawaida hali ambayo ilishika kasi siku chache zilizopita.
Kama mwanao angelikuwepo kwenye kundi hilo, ungelifanyaje!!!?