Kijana mmoja ajulikanaye kwa jina la Chilaga Isaack mkazi wa Yombo Dar es salaam, amejikuta akiiweka ndoa yake katika hali ya hatari baada ya kuchelewa kurudi nyumbani toka kazini kwa sababu ya foleni kubwa ya magari barabarani.
Isaack aliseme kwamba aliporudi nyumbani majira ya saa nne na nusu usiku nyumbani alimkuta mchumba wake amekasirika na alianza kumuuliza maswali ambayo yalimweka kijana huyo kwenye wakati mgumu na wakati huo dada huyo akidai kurudishwa kwao.
"Unajua huyu mchumba wangu anadhani kwamba mimi nilikuwa na mwanamke sehemu fulani wakati haiko hivyo bali ni foleni tu barabarani ndio chanzo cha mimi kuchelewa kurudi", alijitetea Isaack.