Thursday, 16 January 2014

AUAWA NA KUTUPWA SHIMONI.

Mtu mmoja aliyefahamika kwa  jina moja la Lipanje aliyekuwa mlizi wa duka la bwana Time amekutwa amefariki dunia kwenye usiku wa kuamkia jana shimo lililopo nyuma ya msikiti uliopo  nyuma ya duka  hilo katika kijiji cha Mbekenyera wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.

Tukio hilo limetokea baada ya watu  wasiojulikana kuvamia duka hilo usiku wa manane na kuanza kumvamia mlinzi huyo na baadae kuondoka na mali iliyokuwepo dukani humo.

Baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wamelielezea tukio hilo kama tukio la kinyama na wameliomba jeshi la polisi wilayani humo kuwatafuta wahusika wa tukio hilo haraka iwezekanavyo.

"Inakuwa ngumu sana kuyaamini matukio ya kinyama kama haya, yaani binadamu wanageuka na kuwa na roho za kinyama," alisema Evodias clemens

Matukio ya uvamizi wa maduka na  mauaji katika wilaya ya Ruangwa yamekithili kufuatia matukio ya aina hii  kujitokeza mara kwa mara mwaka jana na kusababisha vifo vingi pamoja na hasara kubwa  kwa wamiliki wa maduka.