![]() |
Kwa wale ambao wanatoka nchi za jirani na Korea kama vile uchina wamekuwa wakipata matatizo wakati wanaporudi makwao kwa kukwama kwenye vituo vya usafiri kutokana na nyuso zao kubadilika kupitiliza na kuonekana tofauti na zile zilizopo kwenye vitambulisho vyao vya kusafiria.
Mtandao wa China Daily umelipoti kuwa, mwaka 2009, wachina 23 walikwama uwanja wa ndege walipotaka kurudi kwao kwa kile kilichodaiwa kuwa walikuwa tofauti na picha za vitambulisho vyao hivyo walitiliwa wasiwasi.
Tatizo hilo limekuwa kawaida kiasi cha hospitali zinazotoa huduma za upasuaji kutoa vyeti vya kuwatambulisha wateja wao wanapokwama kwenye vituo vya kusafiria. Via China Daily