Monday, 24 March 2014

Ronaldo atoa ya rohoni, azungumza yake kuhusu mechi ya jana. Twende sote hapa na vitendo ukayaone maneno aliyoyatoa.

"Ulikuwa mchezo mgumu japokuwa kuna baadhi ya watu walikuwa hawataki sisi tushinde au kuwaona Barca nje ya mashindano.

"Nimekuwepo hapa kwa muda mrefu; na ni dhahili kwamba watu wanasumbuliwa na ushindi wa Real siku zote, hii ni klabu kubwa, wanaijenga wivu tukishinda.

"Mwamuzi amefanya makosa mengi sana na inatakiwa apangwe mwamuzi anayeona umuhimu wa mchezo, yule alikuwa na wasiwasi sana na hakutulia.

"Sio kama najiweka upande ulio sahihi, kulikuwa na vitu vingi, baadhi ya watu walikuwa wanataka Barca wabaki kwenye mashindano na kweli wamebaki.

"Penati yangu inaweza kuwa nje ya eneo halali lakini kuna mengi yaliyotokea na ilikuwa ngumu kushinda kwa kuwa wengi hawakutaka tushinde."