Tuesday, 25 March 2014

Ulishawahi kuwa na tabia kama hii wakati unasoma!? Ebu tufuatane na vitendo hapa upate AMSHA AMSHA hii muhimu.

Tabia ya kuwapeleka wazazi bandia shuleni pindi mwanafunzi anapohitajika kumpeleka mzazi shuleni ni tabia ambayo imeenea sana kwa wanafunzi haswa wa sekondari.

Hii utokea pale mwanafunzi anapofanya kosa na kutakiwa kumpeleka mzazi ili apate taarifa kuhusu tabia ya mwanae lakini mwanafunzi utumia njia mbadala kificha maovu yake na kutatua tatizo kwa kukodi mzazi bandia.

Kwa kukodi mzazi, tabia ya mwafunzi haiwezi kubadilika kabisa kwa kuwa mwanafunzi huyu anaendelea kujitengenezea tabia nyingine mbaya ya uongo.

AMKA mwalimu, fanya uchunguzi wa haraka haraka unapoletewa mzazi ili kufahamu kama aliyekuja kuripoti ni mzazi husika ama la. AMKA mwanafunzi, peleka mzazi husika acha kukodi wapita njia maana ni kwa faida yako.