Monday, 24 March 2014

"Unyama unyamani, tutafute pesa kwanza, niite J.M. a.k.a Gaidi: ujumbe ulioachwa na baba baada ya kumnyonga mwanae wa mwaka 1. Ebu twende tuifuatilie hii na vitendo upate mengi.

Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi saba, Henry Juma, amenyongwa na baba yake
mzazi hadi kufa na kisha mwili wake kulazwa kitandani na mtuhumiwa kutokomea
kusikojulikana.

Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya , Ahmed Msangi alisema jana mauaji hayo yalifanyika katika eneo la Migombani katika Mji mdogo wa Tunduma.

Alisema pembeni mwa mwili wa marehemu ulikutwa ujumbe unaosadikiwa kuandikwa na
mtuhumiwa (baba wa mtoto) ukisomeka: Unyama, unyamani, tutafute pesa kwanza, niite J.M. a.k.a Gaidi.’

Alimtaja mtuhumiwa wa mauaji hayo, ambaye Polisi inaendelea kumtafuta kuwa ni Juma Venance.

Inadaiwa alifanya mauaji hayo Machi 22, mwaka huu saa 12 jioni na kisha kufunga mlango kwa
nje kwa kufuli na kutokomea kusikojulikana.

Kwa mujibu wa Kamanda, tetesi juu ya mauaji hayo zilipotolewa, maofisa wa Upelelezi wakishirikiana na raia wema walifika eneo hilo na kisha kuvunja mlango na ndipo wakakuta maiti
ya mtoto akiwa amelazwa kitandani.

Juhudi za kumtafuta mtuhumiwa zinaendelea, kamanda alisema.

Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Ahmed Msangi