Thursday, 2 June 2016

Ni zamu ya Kajala na Quick Rocka kujiachia, mapenzi motomoto tena hadharani

Mapenzi ya Kajala na Quick Rocka yamekuwepo kwa muda sasa lakini hakuna hata mmoja amewahi kukiri hadharani.Hata hivyo penzi linaponoga, si rahisi tena kulificha.

Ndio maana Quick ameamua kushare video Instagram inayomuonesha akipeana mabusu ya haja ya staa huyo wa filamu.

“How I dance HAPO na mama lao……mtoto kapiga 6kichwa mbichi kama mtoto wa shule (Tag her),” ameandika Quick kwenye video hiyo.