Thursday, 2 June 2016

Bado Diamond aendelea kumfanyia Rich Mavoko makubwa

Baada ya Rich Mavoko Alhamisi hii kuandika historia mpya katika maishaya muziki wake kwa kusaini rasmi mkataba wa miaka 10 wa kufanya kazi na label ya ‘WCB’ iliyochini Diamond Platnumz, staa wa huyo wa hit nyingi amekaribishwa rasmi ‘State House’ ya Diamond iliyopo Madale kando kando kidogo ya jiji la Dar es salaam.

Kwa mujibu wa mmoja kati ya viongozi wake WCB, aliimbia Bongo5 kuwa tukio hilo haliitaji maparazi kwani wameliweka kifamilia zaidi.

Hata hivyo Diamond aliona ashare hata video kwa mashabiki wa muziki wake kuonyesha namna walivyompokea msanii huyo.Kwa sasa Rich Mavoko anatamba na video yake mpya ya wimbo ‘stori’ ambayo ilizinduliwa jana baada ya kusaini mkataba na WCB.

Bongo5