Thursday, 2 June 2016

Fisi wafanya fujo makaburini, wafukua makabuli na kusambaza baadhi ya viungo mitaani

Fisi wanadaiwa kufukua baadhi ya makaburi yaliyoko katika Manispaa ya Shinyanga na kuacha miili ya binadamu waliokuwa wamezikwa humo.

Imeelezwa baadhi ya viungo hivyo vimeokotwa katika Mtaa wa Butengwa Kata ya Ngokolo.

Pia, miili mingine ya baadhi ya binadamu imekutwa katika makaburi hayo ikiwa imefunikwa na mifuko ya sandarusi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Mika Nyange alisema tukio hilo lilitokea juzi saa moja asubuhi.

Mwananchi