Friday, 27 May 2016

Waamuliwa kuwavalisha punda nepi ili wasichafue barabara

Kaunti moja ya Kaskazini mashariki mwa Kenya imechukua hatua zisizoza kawaida kulinda barabara moja iliotiwa lami, kwa kuwavalisha nepi punda wanaotumia barabara hiyo.

Mikokoteni yote inayofanya kazi Wajir sasa italazimika kuweka begi nyuma ya wanyama hao ili kuokota kinyesi chao kwa lengo la kuhakikisha barabara iko safi.Ni barabara kuu ya kwanza katika historia ya eneo hilo.

Wakenya wameenda katika mitandao ya kijamii ili kusambaza uvumi vile punda wa Wajir wanapaswa kufuatasheria hiyo mpya mara moja.Hii hapa taarifa iliotolewa na serikaliya eneo hilo:

''Tunashukuru mchango unaoletwa na waendesha mikokoteni ya punda kwa uchumi wa Wajir,hatahivyo,mji huo ni sharti usafishwe kila mara.Kutokana na hilo,mumeagizwakusimamia kinyesi cha punda wenu ili kutochafua barabara.Hakuna Punda atakayeruhusiwa mjini bila mfuko wa kubebea kinyesi kufikia tarehe 29 mwezi Mei''.