Friday, 27 May 2016

Huku kwetu mtu akifumaniwa, kesi yake inamalizwa kwa namna hii ya kipekee

Katika Ya kwetu haya ambayo inakujia kwa ushirikiano na vitendo.blogspot.com inakuketea hii desturi ya kwetu kuhusiana na jinsi watu wa kwetu wanavyotatua tatizo la ugoni.

Ugoni ni tendo la kumfumani au kufumaniwa na mke/mwanaume ambaye sio wako wakiwa wanajihusha na mahusiano ya kama mke na mume.

Tatizo hili lipo kila sehemu. Lakini sasa kila sehemu ina namna yake ya kulitatua tatizo hili pindi linapotokea.

Hivi karibuni kumekuwa na njia maarufu sana ya kutatua mgogoro huu wa fumanizi ambayo imekuwa ikitumika sana katika jiji la Dar na hii ni kumpiga picha aliyefumaniwa na kuzisambaza mitandaoni ikiwa kama adhabu ya aliyefumaniwa.

Lakini huku kwetu hali ni tofauti kabisa...huku kwetu ukifumaniwa basi jiandae kulipa kitita kinono cha pesa kwa aliyekufumania.

Kama umefumaniwa na mke wa mtu basi jipange kulipa pesa isiyopungua laki tano hadi nane. Hii ni kwa wanaume wanaofumaniwa na wake za watu.

Je wanawake waliofumaniwa na waume za watu wanapatiwa adhabu gani?

Hapa mwanamke anahusika katika adhabu lakini si moja kwa moja. Si moja kwa moja ikimaanisha kuwa ataambiwa atoe kiasi fulani cha pesa lakini pesa hiyo haitatoka kwake bali itatoka kwa yule mwanaume aliyekutwa nae japokuwa vichwani mwa watu itaeleweka kama inatoka kwa mwanamke aliyefumaniwa.

Ya kwetu haya katika fumanizi!

Na hiyo ndio adhabu kubwa inayotolewa kwa aliyefumaniwa. Ni mara chache sana kwa anayefumaniwa kukuta amepigwa au kufanywa lolote isipokuwa atatozwa pesa tu.

Kuna siku nilikuwa uhitaji wa kufamu sana iwapo adhabu hii inaweza zuia waliofumaniwa kuendelea au vip, lakini sikujibiwa ipasavyo na mpaka sasa natafuta jibu linalojitosheleza.

Haya ni Ya kwetu haya, je huko kwenu kesi kama hii mnaimalizaje?