Sunday, 29 May 2016

Mwanao akifanya kosa unatumia njia gani kumkanya? Wazazi hawa watumia njia hii ya ajabu kumkanya mtoto wao

Wazazi wa mtoto mvulana wa umri wa miaka saba ambaye hajulikani aliko katika milima iliyo kaskazini mwa Japan wamekiri kuwa walimtelekeza mvulana huyo kama njia ya kumuadhibu.

Mtoto huyo hajaonekana kwa muda wa siku mbili tangu wazazi wake, wamuache katika eneo la Hokkaido, ambapo wanaishi wanyama pori wakiwemo dubu.

Awali wazazi wake waliwaambia polisi kuwa mvulana huyo alitowekawakati walikuwa wakitafuta mboga msituni.

Lakini baadaye walikiri kumtelekezamwanao na kusema kuwa waliporudi kumtafuta dakika tano baadaye walipata ametoweka.

Bbcswahili