Monday, 30 May 2016

'Tunaishi katika kizazi ambacho wapenzi wako huru kushikana sehemu...' Ni sehemu ya Nukuu za Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe kuhusu mapenzi

Ni baadhi ya nukuu za Rais wa Zimbabwa Robert Mugabe zihusuzo mapenzi.

"Bikira ni zawadi pekee kwa mwanaume kutoka kwa mwanamke aliemuoa siku baada ya harusi lakini hivi sasa hakuna kitu kama hicho kwa vile hivisasa zawadi hiyo inapewa kama siku ya kuzaliwa, kusaidia kupata lazi, kununuliwa gari, kupangishiwa nyumba."

"Tunza vizuri kila sehemu ya taulo lako kwa sababu sehemu ya taulo ambayo imefuta makalio yako leo, kesho itafuta uso."

"Tunaishi katika kizazi ambacho wapenzi wako huru kushikana sehemu nyeti, ila sio kushika simu ya mwenzako."

"Muda mwingine unaangalia nyuma kutizama wanawake ambao umetumia pesa zako kuwagharamia badala ya kumtumia mama yako hizo pesa na unaamini kumbe kweli uchawi upo."

"Kama wewe ni mume wa mtu na unajikuta ukivutiwa na wasichana wa shule, mnunulie mkeo sare za shule."

"Kama Rais Barack Obama anataka mimi niruhusu ndoa za jinsia moja katika nchi yangu ya Zimbabwe, aje Zimbabwe ili nimuoe kwanza yeye."

"Msigombanie wanawake! Nchi imejaa wanawakewengi warembo. Kama umeshindwa kumpata mmojawapo njoo kwa Mugabe."

"Sigara ni tumbaku kidogo ambayo imezungushiwa karatasi, ikiwa na moto upande mmoja na mpumbavu katka upande mwingine akivuta."