Sunday, 29 May 2016

Mama aamua kuzichuna na kuzikata sehemu za siri za mtoto wake wa miaka 2

Ule usemi wa mtoto wa mwenzio ni wako, kwa mama huyu umekuwa tofauti na kuamua kumfanyia kitendo kisicho cha kibinadamu mtoto wake wa kiume wa kufikia.

Haya yametokea huko nchini Nigeria ambapo mama huyo aliamua kuzikata na kuzimenya sehemu za siri za mtoto huyo na kuziacha wazi.

Kama hiyo haitoshi basi aliamua kuchukua kisu na kuukata ulimi wa mvulana huyo, mikono, miguu yote kuikata na kumalizia kumtoboa macho yote mawili.

Aliyeposti tukio hilo kupitia mtandao wa twitter YMRigasa amedai kuwa tukio hilo limetokea katika kijiji cha Gulu.

Mtandao wa Pulse Ng umeandika kuwa mvulana huyo kwa sasa amelazwa katika hospitali ya Aminu Kano wakati mwanamke mtendaji wa tukio ameshikiliwa na Polisi kwa uchunguzi.

Alichoposti YMRigasa

"Horror: His step mother cut his tongue, broke his arms and legs, damaged his right eye and castrated him with blade."

MirrowDaily