Friday, 27 May 2016

Kundi la ubakaji laibuka kigoma

Kundi linalotambulika kwajina la Teleza limeibuka mjini Kigoma ambapo linavamia na kuvunja nyumba ambazo hazina wanaume na kuwabaka wanawakeusiku wa manane.

Baadhi ya waathirika wa tukio hilo, wamesema kundi hilo limeibuka wiki mbili zilizopita na limekuwa likiingia katika makazi ya wanawake na kuwafanyia unyama huo huku likitishia kuwajeruhi kwa silaha mbalimbali ikiwamo visu namapanga, iwapo hawatakubali kufanyiwa hivyo.

Mmoja wa wanawake hao mwenyeumri wa miaka 55, amesema alinusurika kubakwa baada ya kupiga kelele.

Diwani wa Kata ya Mwanga Kusini,Mussa Maulid amesema amepokea malalamiko kutoka kwazaidi ya wanawake 12 waliofanyiwa vitendo hivyona baadhi yao wamekuwa wakiogopa kutoa taarifa kwa hofu ya kufanyiwa unyama zaidi na kundi hilo.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Fredinand Mtui amesema wanamshikilia kijana anayedhaniwa kufanya vitendo hivyo na kuwaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa dhidi ya watu wanaojihusisha na vitendo vya udhalilishaji.

“Mpaka sasa tumeshapokea taarifa za wanawake wanne wakidai kufanyiwa unyama huo, hata jana  binti mwenye miaka 20 akiwa amelala na wadogo zake aliingiliwa, baada ya kukataa kutoaushirikiano alijeruhiwa kwa panga mkono wa kulia,” alisema.

Mwananchi