Friday, 27 May 2016

Jokate aka Kidoti afunguka juu ya Baraka Da Prince, akili kumzimia

Mrembo wa nguvu, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ amefunguka kuwa katika orodha ya wasanii wa Bongo Fleva anaowakubali kwa sasa Bongo, Baraka Andrew ‘Baraka Da Prince’ ameuteka vilivyo moyo wake.

Kidoti amefunguka hayo juzikati alipokuwa akipiga stori na mwanahabari wetu ambapo alipoulizwa kuhusu msanii wa Bongo Fleva anayemkubali zaidi, Jokate alisema anamkubali kinomaBaraka Da Prince.

“Yeah! Namkubali sana Baraka, ni mtu ambaye anafanya vizuri kwa kweli ananikosha. Mwingine ni huyuRaymond, naye nampenda,” alisema Jokate, mwanamitindo, mwigizaji na msanii wa Bongo Fleva.

Globalpubliahers