Tuesday, 8 April 2014

Wewe Rihanna, mimba ni ya Drake au Chris!?

Tetesi zilizopo ni kwamba Rihanna ni mjamzito; Mtandao wa Media Take Out umejuzwa na chanzo fulani kuwa  Rihanna ameacha kutumia vilevi wiki kadhaa zilizopita kwa kile kinachosadikiwa kuwa ni mjamzito.

Mtandao huo umedokezwa kuwa, Ri amekuwa akihudhulia maonyesho mbalimbali ya Drake hivi karibuni kwa lengo la kujiweka mbali na utumizi wa marijuana jambo linalotiliwa wasiwasi huenda bibie akawa na kitu tumboni.

Ila licha ya uwepo wa tetesi za kuwa na kitu tumboni bibie huyo alionekana akijirusha ile mbaya kama mtu asiye na kitu tumboni jumapili iliyopita huko Hollywood.

Swali linakuja je, bibie ni mjamzito kweli? Na kama ni kweli, je ni ya Drake au Chris!?