Friday, 11 April 2014

Wanawake 4 wafanikiwa kupandikizwa UKE uliozalishwa maabara.

Wake Forest Institute for Regenerative Medicine

Wanasayansi toka Wake Forest Institute for Regenerative
Medicine wametangaza leo kuwa wamefanikiwa kupandikiza uke kwa wanawake wanne tangu mwaka 2005 hadi 2008 maumbile ambayo yalizalishwa maabara.

Pia wamesema kuwa wanawake wote waliopandikizwa maumbile hayo wanaendea vizuri kutokana na maelezo ya madaktari wanaowahudumia.

Wanawake waliofanyiwa upasuaji wa? kuanzia miaka 13 hadi 18 walizaliwa na maumbile ya ajabu hali ambayo ijulikanayo kama
Mayer-Rokitansky-Kuster-Hauser
syndrome(MRKH), hali inayosababisha mwanamke 1 kati ya 45,000  wanaozaliwa kupatwa na tatizo la kuwa na uke wa ajabu.

Njia iliyokuwa ya kawaida kwa mwanamke anayezaliwa na MRKH ni kuujenga upya uke ili ukae sawa. Matatatizo hayo yamekuwa yakisumbua sana ndio maana watafiti wakaamua kutengeneza uke kama utafiti wa The Lancettoday unavyosema.

Viungo hivyo vya uke walivitengenezwa kutumia muunganiko wa viini vya epithelial, viini vya misuli na viini vya biopsied kutoka kwenye maumbile ya uzazi wa mwanamke.

Anthony Atala, daktari wa maumbile ya wanawake (urologist) katika chuo cha Wake Forest alisema yeye na timu yake walichukua sehemu ndogo ya viini taja hapa juu na kuvitengeneza katika umbo la uke na kufanikiwa kuvikuza na baada ya wiki sita walianza kuwafanyia upasuaji wagonjwa na kuwapandikiza.

Picha ya Uke uliopandikizwa.Omgghana