Rais Goodluck Jonathan agawa iPhones za dhahabu kwa wageni walioudhuria ndoa ya binti yake.
Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan ametoa zawadi ya shukrani ya simu aina ya iPhone kwa kila mgeni mwalikwa aliyeudhulia sherehe ya ndoa ya mwanae wa kike wa kwanza,Faith iliyofanyika Abuja Ecumenical Centre leo.
Ukiachana na mzee Goodluck kutapika simu hizo zenye gharama kwa wageni, pia ndoa hiyo ilikuwa ikirushwa moja kwa moja na kituo cha runinga cha NTA.