Viongozi watatu nchini ambao ni makamu wa Rais, Mohamed Bilali, waziri wa ujenzi, John Magufuli na kamanda wa polisi kanda maalumu jijini Dar, Suleiman Kova muda mfupi uliopita wamenusurika kufa baada ya ndege ya jeshi waliyokuwa wamepanda kupata hitirafu.
Viongozi hao waliokuwa wakipanda ndege hiyo katika uwanja wa ndege wa jeshi Airwing Ukonga jijini Dar kwa lengo la kufanya ukaguzi wa athari za mvua zilizotokea jijini Dar.
Imeripotiwa kuwa hakuna aliyeumia.
Chanzo. Radio One