Wednesday, 16 April 2014

(Picha) Mshabiki wa timu ya taifa ya Brazil avaa mavazi yanayofanana na rangi za bendera ya Brazil kwa miaka 20 ili kutimiza ahadi.

Jamaa anayekwenda kwa jina la Nelson Paviotti, ni mbrazil mwenye mapenzi makubwa sana na timu yake. Nelson aliahidi kuvaa nguo zinazofanana na rangi za bendera ya Brazil endapo itashinda kombe la dunia mwaka 1994, na alianza kufanya hivyo mara baada ya timu hiyo kunyakua ubingwa mwaka huo. Jamaa huyo, kwa miaka 20 sasa amekuwa akivaa mavazi yenye rangi zilizopo kwenye bendera ya nchi yake kama inavyoonekana katika picha. Sio mavazi tu ila kila kitu chake kina rangi hizo. Via Metro