Saturday, 12 April 2014

Mama: Rudisheni uume wa mwanangu.

Mama wa mtoto wa miezi 3, Akua Bemuaba mkazi wa huko Ghana anaidai hospitali ya Juaboso uume wa mtoto wake uliokatwa na mtu asiyejulikana.

Kwame Bemuaba alifariki miezi 3 baada ya kuzaliwa; wazazi wake waligundua kuwa uume wake umekatwa walipokwenda kuchukua maiti sehemu ya kuhifadhia maiti.

Wazazi hao waliamua kuchukua hatua za kisheria dhidi ya hospitali hiyo kutokana na maelezo yao kutojitosheleza juu ya upotevu wa uume wa mtoto huyo.

Mama wa mtoto huyo alisema kuwa watoto wake mapacha walipatwa na homa na kuwapeleka hospitali na ndipo baadae walipotaarifiwa kuwa wote wawili wamefariki dunia.

Ila walipokwenda kufuatilia miili ya watoto wao walikuta mwili wa mtoto mmoja umekatwa uume.

Alisema kuwa, wahusika walikana kufahamu chochote kuhusu upotevu wa uume wa mtoto huyo ndipo walipoamua kuripoti kituo cha polisi.

Akua Bemuaba