Thursday, 10 April 2014

Facebook yatangaza kuwakomesha waomba 'likes', 'share'.

Mtandao wa facebook jana umetangaza njia nyingine tofauti kufanya uchaguzi wa kurasa zinazotangazwa mtandaoni kwa kimpatia mtumiaji chaguzi tofauti kama vile, 'like', 'share', 'coment' au 'ignore'.

Facebook imefikia uamuzi huo kwa lengo la kuondokana na kurasa zilizo na malengo tofauti, kama zile zinazoangaika usiku kucha kuomba 'likes'.

Pia facebook inatarajia kuwaadhibu watumiaji ambao wana tabia ya kuzirudiarudia  'kuzishare' 'post' zao.

Pia facebook inatengeneza njia mahususi ya kuwaadhibu wale wanaotoa 'links' zao zinazowaomba watu 'walike' 'kucoment' kwa lengo kuu la kuwapeleka kwenye 'web' zao zinazotangaza biashara zao, links hizo zimekuwa zikiwatoa watumiaji nje ya facebook.