Wanafunzi wa shule ya Msingi Mwakikonge, wilayani Mkinga wanasomea chini ya miti ya mikorosho kutokana na kukosekana kwa madarasa shuleni hapo.
Shule hiyo yenye wanafunzi 450 ina madarasa mawili, walimu wanne na haina nyenzo muhimu
za kufundishia tangu ilipoanzishwa mwaka 2009.
Akizungumza katika mahojiano,Diwani wa Kata ya Duga, Ali Ali, alisema wanafunzi wa shule hiyo walianza kusoma chini ya mti na mpaka sasa wanafunzi wa darasa la
kwanza mpaka la tano wanasoma chini ya mti nadarasa la sita na la saba tu ndio waliopo madarasani.
“Hii shule inakabiliwa na changamoto nyingi sana ikiwamo ukosefu wa madarasa na waalimu, waalimu waliopo ni wanne tu na
madarasa ni mawili tu na mwaka huu tuna wanafunzi wa darasa la saba tangu shule ilipoanzishwa hatujui matokeo yatakuaje,"alisema Ali.
Hata hivyo, wananchi wa Sweden kupitia mfuko wa Agape Charity, wametoa msaada wa vitabu vya masomo mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 6.8
Vitabu hivyo vilivyotolewa ni vya masomo ya Kiswahili, Historia, Jiografia, Uraia, Stadi za kazi
na kiongozi cha mwalimu kwa masomo yote.