Sunday, 30 March 2014

Nguruwe hana wivu kama wanyama wengine eti, daa ameumbwaje huyu!? Vitendo anakusindikiza hapa, hebu twende.

Ana pua kubwa, macho madogo na
mkia mdogo unaokuwa umejikunja na mfupi, uliopinda au ulonyooka.

Huwa ana mwili mkubwa, miguu mifupi na nywele zilizojiviringisha. Ana kwato nne kwa kila mguu,huku mbili kubwa za mbele anazozitumika kutembelea.

Bila shaka kwa wale wazoefu wa mnyama huyu watakuwa tayari wameshamtambua kuwa ni nani. Si mwingine ni yule ambaye kwa watu fulani ni halamu na kwa wengine ni kitoweo kizuri sana.

Huyu ni Nguruwe maalufu kama kitimoto ambaye anasemekana kutokuwa na wivu kama ilivyo kwa wanyama wengine.

Imezoeleka kuona wanyama kama vile mbuzi, ng'ombe, kondoo na hata ndege kama kuku na bata kuonyesha hisia za wivu kwa wenzi wao, lakini mambo ni tofauti kwa nguruwe.

Inasemekana kuwa mnyama huyu ambaye ni halamu kwa baadhi ya watu kutokuwa na tabia ya kuonyesha wivu pale anapomuona mwenza wake yupo na mwingine jambo linalomfanya hawe wa  tofauti na wanyama wengine.

Nguruwe huwa anakuwa bize kula pale inapotokea mwenza anashiriki na mwingine jambo ambalo ni tofauti kwa mbuzi au kuku ambao huwa wanalinda penzi lao na kulionea wivu.