Tuesday, 4 March 2014

Kwa nini mwanafunzi unakodi mzazi unapotakiwa kupeleka mzazi shuleni!? Hii hapa AMSHA AMSHA na vitendo, fuatilia hapa kufahamu zaidi juu ya wazazi 'feki'.

Tabia ya kuwapeleka wazazi bandia shuleni pindi mwanafunzi anapohitajika kumpeleka mzazi shuleni ni tabia ambayo imeenea sana kwa wanafunzi haswa wa sekondari.

Hii utokea pale mwanafunzi anapofanya kosa na kutakiwa kumpeleka mzazi ili apate taarifa kuhusu tabia ya mwanae lakini mwanafunzi utumia njia mbadala kificha maovu yake na kutatua tatizo kwa kukodi mzazi bandia.

AMKA mwalimu, fanya uchunguzi wa haraka haraka unapoletewa mzazi ili kufahamu kama aliyekuja ni mzazi husika ama la. AMKA mwanafunzi, peleka mzazi husika acha kukodi wapita njia maana ni kwa faida  yako.