Thursday, 13 March 2014

Hofu yamjaa mmiliki wa facebook, ampigia simu Obama kumwelezea hofu yake. Fuatilia hapa na vitendo kufahamu hofu gani aliyonayo Zuckerberg.

Mmiliki wa mtandao wa kijamii wa facebook Mark Zuckerberg amempigia simu Rais wa Marekani, Barack Obama kumwelezea hofu yake juu ya jinsi serikali hiyo inavyotumia mtandao kwenye ulinzi wa nchi.

"Serikali ya Marekani inatakiwa iiendeleze internet na sio kuikwamisha kwa vitisho" zuckerberg  aliandika katika bkog.

"Nimempigia Rais Obama kumwelezea hofu yangu juu ya athari wanazozitengeneza kwetu sote zitakazotukumba hapo baadae", aliandika kwenye ukurasa wake wa facebook.

Haya ni baada ya shirika linalosimamia ulinzi wa nchi ya Marekani (National Security Agency) kutengeneza seva zinazofanana (batili) na za facebook ili kuongeza uwezo wake wa kupata taarifa za kiusalama jambo ambalo ni kitisho kwa wadau wa mitandao.

Zuckerberg alisema kuwa tatizo hilo litachukua muda mpaka kurekebishwa.

Pia alisema kuwa Serikali ya Marekani inapaswa kuwa wazi juu ya wanachokifanya, ama la, watu wake wataifikiria tofauti.

Kitendo cha Marekani kutaka kunasa mawasiliano ya dunia nzima ni jambo ambalo linalochukuluwa kama kuingilia siri binafsi na ni kitisho kwa waendesha mitandao.