Serikali ya China imechapisha picha zilizonaswa na mtambo wake wa satelite zikionyesha mabaki ya kitu kipana kikielea katika bahari ya Kusini mwa China.
Picha hizo zilipigwa siku ya Jumapili, saa ishirini na nne baada ya ndege ya abiria ya Malaysia
kutoweka ikiwa na abiria 239, lakini haijabainika kama vifaa hivyo ni vya ndege hiyo.