Tuesday, 4 March 2014

Hivi ni sawa mzazi kumshirikisha mtoto kwenye mbinu za kusema uongo? Hii hapa AMSHA AMSHA na vitendo, ifuatilie hapa kufahamu zaidi juu ya hili.

Wapo wazazi ambao wanamtayarishia mtoto tabia ya uongo kwa kumshirikisha kwenye baadhi ya mbinu za uongo, jambo linalomfanya mtoto aizoee tabia hiyo na kujikuta anakua nayo.

Huwa inatokea mara nyingi pale ambapo mzazi anapomwambia mtoto aseme uongo kwa kumficha mzazi ili kuepuka jambo fulani, wakati huo huo bila kutambua, mzazi anapandikiza sumu za uongo itakayomfanya awe muongo kupindukia daima.

AMKA mzazi, acha kumshirikisha mtoto kwenye uongo, mjengee mtoto tabia njema ya kuwa mkweli kwa kila jambo. Ukimjengea mwanao tabia ya kuwa mkweli basi unakijengea kizazi kijacho tabia safi.