Vijana wa kijiji cha Mbekenyera wilaya ya Ruangwa mkoa wa Lindi wameamua kuendesha harambee kuwachangia waathirika wa kimbunga kijijini humo.
Harambee hiyo imeanzishwa kufuatia mvua kali iliyoambatana na upepo mkali kuezua paa za nyumba za wakazi wa kijiji hicho na kuwaacha bila makazi na kukosa huduma muhimu za kijamii.
Nyumba zipatazo 201 zimeharibiwa na mvua iliyoambatana na upepo mkali iliyotokea siku nne zilizopita.
Mmoja wa vijana hao walisema, wameamua kuendesha harambee hiyo kutokana na uhitaji mkubwa wa huduma za kijamii kwa waathirika.
Hapo chini ni baadhi ya paa za nyumba zilizoezuliwa na kimbunga.