Thursday, 13 February 2014

BELGIUM, WATOTO WAPEWA HAKI YA KUFA,WAPEWA HAKI YA KUAMUA KUKATISHA MAISHA WAKIZIDIWA NA UGONJWA.

Bergium imekuwa nchi ya kwanza duniani kupitisha muswada wa sheria unaompa mtoto aliye chini ya umri 18 haki ya kufa (euthanasia).

Sheria hiyo inampatia mtoto haki ya kuomba kufa (euthanasia) endapo mtoto huyo atakuwa amezidiwa na ugonjwa wenye maumivu makali na wazazi watatakiwa kukubaliana na maamuzi hayo.

Muswada huo ulipigiwa kura ya ndio 86 na hapana 44 na 12 hawakupiga kura.

Ni miaka 12 sasa tangu Belgium ilipoalalisha haki ya kufa (euthanasia) kwa watu wazima.

Chanzo, CNN.